8 Maana alisema:“Je, si kweli majemadari wangu ni wafalme?
9 Je, si kweli kwamba Kalno nitautenda kama Karkemishi,mji wa Hamathi kama mji wa Arpadi,Samaria kama Damasko?
10 Kama nimefaulu kuunyosha mkono wangudhidi ya falme zenye sanamu za miungukubwa kuliko sanamu za Yerusalemu na Samaria;
11 je, nitashindwa kuutenda Yerusalemu na sanamu zake,kama nilivyoutenda Samaria na sanamu zake?”
12 Wakati Mwenyezi-Mungu atakapomaliza kazi zake zote mlimani Siyoni na mjini Yerusalemu, atamwadhibu mfalme wa Ashuru, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake.
13 Maana mfalme wa Ashuru alisema:“Kwa nguvu zangu mwenyewe nimetenda hayo,na kwa hekima yangu, maana mimi ni mwerevu!Nimeondoa mipaka kati ya mataifa,nikazipora hazina zao;kama fahali nimewaporomosha walioketia viti vya enzi.
14 Kama mtu anyoshaye mkono kwenye kiota,ndivyo nilivyochukua mali yao;kama mtu aokotavyo mayai yaliyoachwa kiotani,ndivyo nilivyowaokota duniani kote,wala hakuna mtu aliyeweza kupiga bawa,au aliyefungua kinywa kunipigia kelele.”Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: