23 Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
24 Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa:“Kama nilivyopanga,ndivyo itakavyokuwa;kama nilivyokusudia,ndivyo itakavyokamilika.
25 Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu;nitawakanyagakanyaga katika milima yangu.Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao,na mzigo wa mateso yao.”
26 Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungukuhusu dunia yote;hii ndiyo adhabu atakayotoajuu ya mataifa yote.
27 Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua,nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake?Kama amepania kutoa adhabu,ni nani atakayempinga?
28 Mwaka alipofariki mfalme Ahazi, Mungu alitoa kauli hii:
29 “Msishangilie enyi Wafilisti wote,kwamba Ashuru, fimbo iliyowapiga, imevunjika;maana, nyoka wa kawaida atazaa nyoka mwenye sumu,na nyoka mwenye sumu atazaa joka lirukalo.