1 Ole wao wale waendao Misri kuomba msaada,ole wao wanaotegemea farasi,wanaotegemea wingi wa magari yao ya vita,na nguvu za askari wao wapandafarasi,nao hawamtegemei Mtakatifu wa Israeli,wala hawamwombi Mwenyezi-Mungu shauri!
2 Mungu ni mwenye busara na huleta maangamizi.Habadilishi tamko lake;ila yuko tayari kuwakabili watu waovukadhalika na wasaidizi wa watendao mabaya.
3 Wamisri ni binadamu tu wala si Mungu;farasi wao nao ni wanyama tu, si roho.Mwenyezi-Mungu akiunyosha mkono wake,taifa linalotoa msaada litajikwaa,na lile linalosaidiwa litaanguka;yote mawili yataangamia pamoja.
4 Mwenyezi-Mungu aliniambia:“Kama vile simba au mwanasimba angurumavyokuyakinga mawindo yake,hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili,yeye hatishiki kwa kelele zao,wala hashtuki kwa sauti zao.Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshikupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.
5 Kama ndege arukavyo juu ya viota vyake,ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyoulinda Yerusalemu,ataulinda na kuukomboa,atauhifadhi na kuuokoa.