1 Kutatokea mfalme atakayetawala kwa uadilifu,nao viongozi wataongoza kwa kufuata haki.
2 Kila mmoja atakuwa kama mahali pa kujikinga na upepo,kama mahali pa kujificha wakati wa tufani.Watakuwa kama vijito vya maji katika nchi kame,kama kivuli cha mwamba mkubwa jangwani.
3 Macho hayatafumbwa tena,masikio yatabaki wazi.
4 Wafanyao mambo kwa hamaki wataamua kwa busara,wenye kigugumizi wataongea sawasawa.