3 Kwa kishindo cha sauti yako watu hukimbia;unapoinuka tu, mataifa hutawanyika.
4 Maadui zao wanakusanya mateka,wanayarukia kama panzi.
5 Mwenyezi-Mungu ametukuka,yeye anaishi juu mbinguni.Ameujaza Siyoni haki na uadilifu.
6 Enyi watu wa Yerusalemu,Mwenyezi-Mungu atawajalieni usalama,atawaokoa na kuwapa hekima na maarifa.Hazina yenu kuu ni kumcha Mwenyezi-Mungu.
7 Haya, mashujaa wao wanalia,wajumbe wa amani wanaomboleza.
8 Barabara kuu zimebaki tupu;hamna anayesafiri kupitia humo.Mikataba inavunjwa ovyo,mashahidi wanadharauliwa.Hamna anayejali tena maisha ya binadamu.
9 Nchi inaomboleza na kunyauka;misitu ya Lebanoni imekauka,bonde zuri la Sharoni limekuwa jangwa,huko Bashani na mlimani Karmelimiti imepukutika majani yake.