10 Basi, usiogope, mimi nipo pamoja nawe.Usifadhaike, mimi ni Mungu wako.Nitakuimarisha na kukusaidia;nitakulinda kwa mkono wangu wa ushindi.
11 “Naam! Wote waliokuwakia hasira,wataaibishwa na kupata fedheha.Wote wanaopingana nawe,watakuwa si kitu na kuangamia.
12 Utawatafuta hao wanaopingana nawe,lakini watakuwa wameangamia.
13 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,ndimi ninayetegemeza mkono wako.Mimi ndimi ninayekuambia:‘Usiogope, nitakusaidia.’”
14 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wa Yakobo dhaifu kama mdudu,enyi Waisraeli, msiogope!Mimi Mwenyezi-Mungu nasema nitawasaidia.Mimi ni Mkombozi wenu,Mtakatifu wa Israeli.
15 Nitawafanya muwe kama chombo cha kupuria,chenye meno mapya na makali.Mtaipura milima na kuipondaponda;vilima mtavisagasaga kama makapi.
16 Mtaipepeta milima hiyo,nao upepo utaipeperushia mbali,naam, dhoruba itaitawanya huko na huko.Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu;mtaona fahari kwa sababu yanguMungu Mtakatifu wa Israeli.