12 Utawatafuta hao wanaopingana nawe,lakini watakuwa wameangamia.
13 Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,ndimi ninayetegemeza mkono wako.Mimi ndimi ninayekuambia:‘Usiogope, nitakusaidia.’”
14 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Enyi watu wa Yakobo dhaifu kama mdudu,enyi Waisraeli, msiogope!Mimi Mwenyezi-Mungu nasema nitawasaidia.Mimi ni Mkombozi wenu,Mtakatifu wa Israeli.
15 Nitawafanya muwe kama chombo cha kupuria,chenye meno mapya na makali.Mtaipura milima na kuipondaponda;vilima mtavisagasaga kama makapi.
16 Mtaipepeta milima hiyo,nao upepo utaipeperushia mbali,naam, dhoruba itaitawanya huko na huko.Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu;mtaona fahari kwa sababu yanguMungu Mtakatifu wa Israeli.
17 “Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate,wakiwa wamekauka koo kwa kiu,mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu;mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha.
18 Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu,na chemchemi katika mabonde.Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji,na nchi kame kuwa chemchemi za maji.