20 Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
21 Pia nitawachagua baadhi yao kuwa makuhani na baadhi yao kuwa Walawi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
22 “Kama vile mbingu mpya na dunia mpya nitakazoumbazitakavyodumu milele kwa uwezo wangu,ndivyo wazawa wako na jina lako litakavyodumu.
23 Katika kila sikukuu ya mwezi mpya,na katika kila siku ya Sabato,binadamu wote watakuja kuniabudu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
24 “Kisha watakwenda kuziona maiti za wale walioniasi. Wadudu watakaowala hawatakufa, na moto utakaowachoma hautazimika kamwe. Watakuwa chukizo kwa watu wote.”