6 Kijito cha Nimrimu kimekauka;nyasi zimekauka, majani mabichi yamenyauka,hakuna chochote kinachoota hapo.
7 Watu wanavuka kijito cha Mierebiwamebeba mali yao yote waliyochuma,na kila walichojiwekea kama akiba.
8 Kilio kimezuka pote nchini Moabu,maombolezo yao yamefika Eglaimu,naam, yamefika mpaka Beer-elimu.
9 Maji ya Diboni yamejaa damu,lakini Mungu ataongeza msiba wa Diboni.Hao wachache watakaobaki haina kukimbia kutoka nchini Moabu,watapelekewa simba wa kuwaua.