1 Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri.“Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasina kuja mpaka nchi ya Misri.Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake,mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu.
2 Mimi nitawachochea Wamisri wagongane:Ndugu na ndugu yake,jirani na jirani yake,mji mmoja na mji mwingine,mfalme mmoja na mfalme mwingine.
3 Nitawaondolea Wamisri uhodari wao,nitaivuruga mipango yao;watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu,wachawi, mizuka na pepo.
4 Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana katili,mfalme mkali ambaye atawatawala.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nimenena.”
5 Maji ya mto Nili yatakaushwa,nao utakauka kabisa.