10 Ingieni katika mwamba,mkajifiche mavumbini,kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu,mbali na utukufu wa enzi yake.
11 Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa,majivuno ya kila mtu yatavunjwa;na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.
12 Naam, yaja siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshidhidi ya wenye kiburi na majivuno,dhidi ya wote wanaojikweza;
13 dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni,ambayo ni mirefu na mizuri,dhidi ya mialoni yote nchini Bashani;
14 dhidi ya milima yote mirefu,dhidi ya vilima vyote vya juu;
15 dhidi ya minara yote mirefu,dhidi ya kuta zote za ngome;
16 dhidi ya meli zote za Tarshishi,na dhidi ya meli zote nzuri.