21 Humo Mwenyezi-Mungu atatuonesha ukuu wake.Kutakuwa na mito mikubwa na vijito,ambamo meli za vita hazitapita,wala meli kubwa kuingia.
22 Maana Mwenyezi-Mungu ni hakimu wetu,yeye ni mtawala wetu;Mwenyezi-Mungu ni mfalme wetu,yeye ndiye anayetuokoa.
23 Ewe Siyoni, kamba zako zimelegea,haziwezi kushikilia matanga yake,wala kuyatandaza.Lakini nyara nyingi zitagawanywa;hata vilema wataweza kuchukua sehemu yao.
24 Hakuna atakayesema tena ni mgonjwa;watu watasamehewa uovu wao wote.