11 Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu,katika nchi ya walio hai;wala sitamwona mtu yeyote tena,miongoni mwa wakazi wa ulimwengu.
12 Makao yangu yamengolewa kwangu,kama hema la mchungaji;kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu;Mungu amenikatilia mbali;kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.
13 Usiku kucha nililia kuomba msaada;kama simba, anavunjavunja mifupa yangu;mchana na usiku ananikomesha.
14 “Ninalia kama mbayuwayu,nasononeka kama njiwa.Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu.Ee Bwana, nateseka;uwe wewe usalama wangu!
15 Lakini niseme nini:Yeye mwenyewe aliniambia,naye mwenyewe ametenda hayo.Usingizi wangu wote umenitorokakwa sababu ya uchungu moyoni mwangu.
16 “Ee Bwana, Sisi twaishi kutokana na yote uliyotenda,kwa hayo yote mimi binafsi pia ninaishi.Nirudishie afya, uniwezeshe kuishi.
17 Nilipata mateso makali kwa faida yangu;lakini umeyaokoa maisha yangukutoka shimo la uharibifu,maana umezitupa dhambi zangu nyuma yako.