8 Nitafanya kivuli kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi, kirudi nyuma hatua kumi.” Nacho kivuli kikarudi nyuma hatua kumi.
9 Kisha mfalme Hezekia alipopona, akatunga wimbo huu wa shukrani:
10 “Nilisema: Nikiwa mbichi kabisa,inanibidi niage dunia.Mimi nimepangiwa kwenda kuzimusiku zote zilizonibakia.
11 Nilisema sitamwona tena Mwenyezi-Mungu,katika nchi ya walio hai;wala sitamwona mtu yeyote tena,miongoni mwa wakazi wa ulimwengu.
12 Makao yangu yamengolewa kwangu,kama hema la mchungaji;kama, mfumanguo nimefungasha maisha yangu;Mungu amenikatilia mbali;kabla hata mwisho wa siku amenikomesha.
13 Usiku kucha nililia kuomba msaada;kama simba, anavunjavunja mifupa yangu;mchana na usiku ananikomesha.
14 “Ninalia kama mbayuwayu,nasononeka kama njiwa.Macho yangu yamefifia kwa kuangalia juu.Ee Bwana, nateseka;uwe wewe usalama wangu!