15 Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo,ni kama vumbi juu ya mizani.Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.
16 Kuni zote za Lebanonina wanyama wake wotehavitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.
17 Mataifa yote si kitu mbele yake;kwake ni vitu duni kabisa na batili.
18 Mtamlinganisha Mungu na nini basi,au ni kitu gani cha kumfananisha naye?
19 Je, anafanana na kinyago?Hicho, fundi hukichonga,mfua dhahabu akakipaka dhahabu,na kukitengenezea minyororo ya fedha!
20 Au ni sanamu ya mti mgumu?Hiyo ni ukuni mtu anaochagua,akamtafuta fundi stadi,naye akamchongea sanamu imara!
21 Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Je, hamkuambiwa tangu mwanzo?Je, hamjafahamu mwanzo wa dunia?