2 Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole,waambieni kwamba utumwa wao umekwisha,wamesamehewa uovu wao.Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufukwa sababu ya dhambi zao zote.”
3 Sauti ya mtu anaita jangwani:“Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia,nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.
4 Kila bonde litasawazishwa,kila mlima na kilima vitashushwa;ardhi isiyo sawa itafanywa sawa,mahali pa kuparuza patalainishwa.
5 Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa,na watu wote pamoja watauona.Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
6 Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!”Nami nikauliza, “Nitangaze nini?”Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani;uthabiti wao ni kama ua la shambani.
7 Majani hunyauka na ua hufifia,Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.Hakika binadamu ni kama majani.
8 Majani hunyauka na ua hufifia,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”