4 Kila bonde litasawazishwa,kila mlima na kilima vitashushwa;ardhi isiyo sawa itafanywa sawa,mahali pa kuparuza patalainishwa.
5 Kisha utukufu wa Mwenyezi-Mungu utafunuliwa,na watu wote pamoja watauona.Mwenyezi-Mungu mwenyewe ametamka hayo.”
6 Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!”Nami nikauliza, “Nitangaze nini?”Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani;uthabiti wao ni kama ua la shambani.
7 Majani hunyauka na ua hufifia,Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.Hakika binadamu ni kama majani.
8 Majani hunyauka na ua hufifia,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”
9 Nenda juu ya mlima mrefu,ewe Siyoni, ukatangaze habari njema.Paza sauti yako kwa nguvu,ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema.paza sauti yako bila kuogopa.Iambie miji ya Yuda:“Mungu wenu anakuja.”
10 Bwana Mungu anakuja na nguvu,kwa mkono wake anatawala.Zawadi yake iko pamoja naye,na tuzo lake analo.