16 Mtaipepeta milima hiyo,nao upepo utaipeperushia mbali,naam, dhoruba itaitawanya huko na huko.Nanyi mtafurahi kwa sababu yangu Mwenyezi-Mungu;mtaona fahari kwa sababu yanguMungu Mtakatifu wa Israeli.
17 “Maskini na fukara wakitafuta maji wasipate,wakiwa wamekauka koo kwa kiu,mimi Mwenyezi-Mungu nitawajibu;mimi Mungu wa Israeli, sitawaacha.
18 Nitabubujisha mito kwenye milima mikavu,na chemchemi katika mabonde.Nitaigeuza nyika kuwa bwawa la maji,na nchi kame kuwa chemchemi za maji.
19 Nitapanda miti huko nyikani:Mierezi, mikakaya, mijohoro, na mizeituni;nitaweka huko jangwani:Miberoshi, mivinje na misonobari.
20 Watu wataona jambo hilo,nao watatambua na kuelewa kwambamimi Mwenyezi-Mungu nimetenda hayo,mimi Mtakatifu wa Israeli nimefanya jambo hilo.”
21 Mwenyezi-Mungu, Mfalme wa Yakobo, asema:“Enyi miungu ya mataifa,njoni mtoe hoja zenu!
22 Leteni hoja zenu, mtuambie yatakayotukia.Tuambieni matukio ya kwanza yalikuwa yapinasi tutayatafakari moyoni.Au tutangazieni yajayo,tujue yatakayokuja.