9 Tazama, mambo niliyotabiri yametukia;na sasa natangaza mambo mapya,nakueleza hayo kabla hayajatukia.”
10 Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya!Dunia yote iimbe sifa zake:Bahari na vyote vilivyomo,nchi za mbali na wakazi wake;
11 jangwa na miji yake yote ipaaze sauti,vijiji vya wakazi wa Kedari vimsifu,wakazi wa Sela waimbe kwa shangwe;wapaaze sauti kutoka mlimani juu.
12 Wote wakaao nchi za mbali,na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu.
13 Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa;kama askari vitani ajikakamua kupigana.Anapaza sauti kubwa ya vita,na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake.
14 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza,nimekaa kimya na kujizuia;lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua,anayetweta pamoja na kuhema.
15 Nitaharibu milima na vilima,na majani yote nitayakausha.Mito ya maji nitaigeuza kuwa nchi kavu,na mabwawa ya maji nitayakausha.