3 “Sikilizeni enyi wazawa wa Yakobo,nisikilizeni enyi mabaki ya watu wangu wa Israeli.Mimi niliwatunzeni tangu mlipozaliwa;niliwabebeni tangu tumboni mwa mama yenu.
4 Mimi ni yuleyule hata katika uzee wenu;hata katika uzee wenu mimi nitawabeba.Nilifanya hivyo kwanza,nitafanya hivyo tena.Nitawabeba nyinyi na kuwaokoa.
5 “Mtanifananisha na nani, tufanane?Je, mwaweza kunilinganisha na nani, tulingane?
6 Watu humimina dhahabu kutoka mifuko yao,hupima fedha kwenye mizani zao,wakamwajiri mfua dhahabu atengeneze sanamukisha huisujudu na kuiabudu!
7 Hujitwisha sanamu hiyo mabegani, wakaibeba,kisha huiweka mahali pake, ikakaa papo hapo;kamwe haiwezi hata kusogea kutoka hapo ilipo.Mtu akiililia, haiwezi kumwitikia,wala haiwezi kumwokoa mtu katika taabu zake.
8 “Kumbukeni jambo hili na kutafakari,liwazeni akilini mwenu enyi wakosefu.
9 Kumbukeni mambo niliyotenda hapo kale!Mimi ndimi Mungu na hakuna mwingine;naam, mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine kama mimi.