2 Twaa mawe ya kusagia, usage unga kama mtumwa!Vua utaji wako, ukavue na mavazi yako!Pandishia vazi lako miguuni, ukavuke mito.
3 Watu watauona uchi wako;naam, wataiona aibu yako.Mimi nitalipiza kisasi,wala sitamhurumia yeyote.”
4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu asema:“Ewe taifa la Wakaldayolililo kama binti mzuri,keti kimya na kutokomea gizani.Maana umepoteza hadhi yakoya kuwa bimkubwa wa falme.
6 Niliwakasirikia watu wangu Israeli,nikawafanya watu wangu kuwa haramu.Niliwatia mikononi mwako,nawe hukuwaonea huruma;na wazee uliwatwisha nira nzito mno.
7 Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’,nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea,wala kufikiri mwisho wake.
8 “Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa,wewe unayedhani kuwa u salama,na kujisemea: ‘Ni mimi tu,na hakuna mwingine isipokuwa mimi.Kamwe sitakuwa mjane,wala sitafiwa na wanangu.’