4 Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu asema:“Ewe taifa la Wakaldayolililo kama binti mzuri,keti kimya na kutokomea gizani.Maana umepoteza hadhi yakoya kuwa bimkubwa wa falme.
6 Niliwakasirikia watu wangu Israeli,nikawafanya watu wangu kuwa haramu.Niliwatia mikononi mwako,nawe hukuwaonea huruma;na wazee uliwatwisha nira nzito mno.
7 Ulijisemea moyoni: ‘Nitakuwa malkia milele’,nawe hukuyatafakari mambo yanayotokea,wala kufikiri mwisho wake.
8 “Sasa, basi, sikiliza ewe mpenda anasa,wewe unayedhani kuwa u salama,na kujisemea: ‘Ni mimi tu,na hakuna mwingine isipokuwa mimi.Kamwe sitakuwa mjane,wala sitafiwa na wanangu.’
9 Haya yote mawili yatakupata,ghafla, katika siku moja:Kupoteza watoto wako na kuwa mjane,ijapokuwa una wingi wa uchawi wako,na nguvu nyingi za uganga wako.
10 “Ulijiona salama katika uovu wako;ukajisemea, ‘Hakuna mtu anayeniona.’Hekima na elimu yako vilikupotosha,ukajisemea moyoni mwako, ‘Mimi ndiye;hakuna mwingine anayenishinda.’