1 Nani aliyeamini mambo tuliyosikia?Nani aliyetambua kuwa mkono wa Mwenyezi-Mungu ulihusika?
2 Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu,mtumishi wake alikua kama mti mchanga,kama mzizi katika nchi kavu.Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza,wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu,alikuwa mtu wa uchungu na huzuni.Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu;alidharauliwa na tukamwona si kitu.
4 Hata hivyo alivumilia majonzi yetu,na kubeba huzuni zetu.Sisi tulifikiri amepata adhabu,amepigwa na Mungu na kuteswa.
5 Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu,aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu.Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai;kwa kupigwa kwake sisi tumepona.