2 Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu,mtumishi wake alikua kama mti mchanga,kama mzizi katika nchi kavu.Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza,wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu,alikuwa mtu wa uchungu na huzuni.Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu;alidharauliwa na tukamwona si kitu.
4 Hata hivyo alivumilia majonzi yetu,na kubeba huzuni zetu.Sisi tulifikiri amepata adhabu,amepigwa na Mungu na kuteswa.
5 Lakini alijeruhiwa kwa sababu ya dhambi zetu,aliumizwa kwa sababu ya maovu yetu.Kwa kuadhibiwa kwake sisi tumepata uhai;kwa kupigwa kwake sisi tumepona.
6 Sisi sote tumepotea kama kondoo,kila mmoja wetu ameelekea njia yake.Lakini Mwenyezi-Mungu alimtwika adhabu,ambayo sisi wenyewe tuliistahili.
7 Alidhulumiwa na kuteswa,lakini alivumilia kwa unyenyekevu,bila kutoa sauti hata kidogo.Alikuwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni,kama kondoo akaavyo kimya anapokatwa manyoya.Hakutoa sauti hata kidogo.
8 Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa;na hakuna mtu aliyejali yanayompata.Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai,kwa sababu ya makosa ya watu wangu.