1 Mnamo mwaka aliofariki mfalme Uzia, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu na cha fahari. Pindo la vazi lake lilienea hekaluni mote,
2 na juu yake walikuwa wamekaa malaika. Kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Mawili ya kufunika uso, mawili ya kufunika mwili na mawili ya kurukia.
3 Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi:“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu,ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi!Dunia yote imejaa utukufu wake.”
4 Sauti yao iliitikisa misingi ya milango ya hekalu, nalo likajaa moshi.