8 Hata hivyo, ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni Baba yetu.Sisi ni kama udongo, wewe ni mfinyanzi.Sisi sote ni kazi ya mikono yako.
9 Usitukasirikie mno, ee Mwenyezi-Mungu,usiukumbuke uovu wetu daima!Ukumbuke kwamba sisi sote ni watu wako!
10 Miji yako mitakatifu imekuwa nyika;Siyoni umekuwa mahame,Yerusalemu umekuwa uharibifu.
11 Nyumba yetu takatifu na nzuri,ambamo wazee wetu walikusifu,imeteketezwa kwa moto.Mahali petu pote pazuri pamekuwa magofu.
12 Je, kwa hayo yote utajizuia usifanye kitu?Je, utaendelea kunyamaza tu, ee Mwenyezi-Mungu,na kututesa kupita kiasi?