3 Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi;hutambikia miungu yao katika bustani,na kuifukizia ubani juu ya matofali.
4 Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku.Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.
5 Huwaambia wale wanaokutana nao:‘Kaeni mbali nami;msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’Watu hao wananikasirisha mno,hasira yangu ni kama moto usiozimika.
6 “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni,sitanyamaza bali nitawafanya walipe;nitawafanya walipe kwa wingi.
7 Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”
8 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri,watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;sitawaangamiza wote.
9 Nitawajalia watu wa Yakobo,na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu;watumishi wangu watakaa huko.