4 Basi, nitawaletea taabu;yatawapata yaleyale wanayoyahofia;maana nilipoita hakuna aliyeitika,niliponena hawakusikiliza.Bali walifanya yaliyo maovu mbele yangu,walichagua yale ambayo hayanipendezi.”
5 Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,enyi msikiao neno lake mkatetemeka:“Ndugu zenu ambao wanawachukia,na kuwapiga marufuku kwa sababu yangu,wamesema kwa dharau‘Mungu na aoneshe utukufu wake,nasi tuwaone nyinyi mkishinda!’Lakini wao wenyewe ndio watakaoaibishwa!
6 Sikilizeni, ghasia kutoka mjini,sauti kutoka hekaluni!Hiyo ni sauti ya Mwenyezi-Munguakiwaadhibu maadui zake!
7 “Mji wangu mtakatifu,ni kama mama ajifunguaye bila kuona uchungu;kabla uchungu kuanza, amekwisha zaa mtoto.
8 Ni nani aliyepata kusikia jambo kama hilo?Ni nani aliyewahi kuona jambo kama hilo?Je, nchi nzima yaweza kuzaliwa siku moja?Je, taifa zima laweza kuzaliwa mara moja?Maana Siyoni, mara tu alipoanza kuona uchungu,alijifungua watoto wake.
9 Je, nitawatunza watu wangu mpaka karibu wazaliwe,halafu niwazuie wasizaliwe?Au mimi mwenye kuwajalia watoto,nitafunga kizazi chao?Mimi Mungu wenu nimesema.”
10 Shangilieni na kufurahi pamoja na Yerusalemu enyi mnaoupenda!Shangilieni pamoja nao enyi nyote mlioulilia!