1 Ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki,watu wanaopitisha sheria za kukandamiza.
2 Huwanyima maskini haki zao,na kuwaibia maskini wa watu wangu maslahi yao.Wajane wamekuwa nyara kwao;yatima wamekuwa mawindo yao.
3 Je, mtafanya nini siku ya adhabu,siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali?Mtamkimbilia nani kuomba msaada?Mtakwenda wapi kuweka mali yenu?
4 Litakalowabakia ni kujikunyata kati ya wafungwana kuangamia pamoja na wanaouawa vitani.Hata hivyo, hasira ya Mwenyezi-Mungu haijatulia,bado ameunyosha mkono wake.
5 Ole wake Ashuru, fimbo ya hasira yangu,yeye ashikaye kiboko cha hasira yangu!
6 Nilimtuma kuliadhibu taifa ovu,nilimwamuru kuwaadhibu watu niliowakasirikia,kuwapora na kuteka nyara,na kuwakanyaga chini kama tope njiani.
7 Lakini Ashuru hakudhamiria hivyo,yeye alikuwa na nia nyingine;alikusudia kuharibu kabisa,kuangamiza mataifa mengi iwezekanavyo.