2 Roho ya Mwenyezi-Mungu itakaa kwake,roho ya hekima na maarifa,roho ya shauri jema na nguvu,roho ya ujuzi na ya kumcha Mwenyezi-Mungu.
3 Atafurahia kumcha Mwenyezi-Mungu.Hatahukumu kadiri ya mambo ya njenje,wala kuamua kufuatana na yale anayosikia.
4 Atawapatia haki watu maskini,atawaamulia sawasawa wanyonge nchini.Kwa neno lake ataiadhibu dunia,kwa tamko lake atawaua waovu.
5 Haki itakuwa kama mkanda wa kujifunga,uaminifu utakaa naye kama mkanda kiunoni.
6 Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo,chui watapumzika pamoja na mwanambuzi.Ndama na wanasimba watakula pamoja,na mtoto mdogo atawaongoza.
7 Ngombe na dubu watakula pamoja,ndama wao watapumzika pamoja;na simba atakula majani kama ng'ombe.
8 Mtoto mchanga atacheza kwenye shimo la nyokamtoto ataweza kutia mkono shimoni mwa nyoka wa sumu.