1 Siku hiyo mtasema:“Nakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu,maana ingawa ulinikasirikia,hasira yako imetulia,nawe umenifariji.
2 Mungu ndiye mwenye kuniokoa,nitamtegemea yeye, wala sitaogopa;Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu;yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.”
3 Mtachota maji kwa furahakutoka visima vya wokovu.
4 Siku hiyo mtasema:“Mshukuruni Mwenyezi-Mungumwombeni kwa jina lake.Yajulisheni mataifa matendo yake,tangazeni kuwa jina lake limetukuka.