1 Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Moabu.Mji wa Ari nchini Moabu umeangamizwa usiku;mji wa Kiri nchini Moabu umeteketezwa usiku.
2 Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza,watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba;vichwa vyote vimenyolewa upara,ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
3 Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia.Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mjiwatu wanalia na kukauka kwa machozi.
4 Watu wa Heshboni na Eleale wanalia,sauti zao zinasikika hadi Yahazi.Hata askari wa Moabu wanalia kwa sauti;mioyo yao inatetemeka.