2 Mimi nitawachochea Wamisri wagongane:Ndugu na ndugu yake,jirani na jirani yake,mji mmoja na mji mwingine,mfalme mmoja na mfalme mwingine.
3 Nitawaondolea Wamisri uhodari wao,nitaivuruga mipango yao;watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu,wachawi, mizuka na pepo.
4 Nitawatia Wamisri mikononi mwa bwana katili,mfalme mkali ambaye atawatawala.Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, nimenena.”
5 Maji ya mto Nili yatakaushwa,nao utakauka kabisa.
6 Mifereji yake itatoa uvundo,vijito vyake vitapunguka na kukauka.Nyasi na mafunjo yake yataoza.
7 Sehemu za kandokando ya Nili zitakuwa tupu.Mimea yote iliyopandwa humo itakaukana kupeperushiwa mbali na kutoweka.
8 Wavuvi watalia na kuomboleza,wote watumiao ndoana watalalama;wote wanaotanda nyavu majini watakufa moyo.