2 Nyamazeni kwa mshangao enyi wakazi wa pwani,naam, tulieni enyi wafanyabiashara wa Sidoni,ambao wajumbe wenu wanapita baharini,
3 wakasafiri katika bahari nyingi.Mapato yenu yalikuwa nafaka ya Misri,mkaweza kufanya biashara na mataifa.
4 Aibu kwako ewe Sidoni,mji wa ngome kando ya bahari!Bahari yenyewe yatangaza:“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa,wala sijawahi kuzaa;sijawahi kulea wavulana,wala kutunza wasichana!”
5 Habari zitakapoifikia Misrikwamba Tiro imeangamizwa,Wamisri watafadhaika sana.
6 Ombolezeni enyi wenyeji wa Foinike!Jaribuni kukimbilia Tarshishi.
7 Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro,mji ambao ulijengwa zamani za kale,ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali?
8 Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro,mji uliowatawaza wafalme,wafanyabiashara wake walikuwa wakuu,wakaheshimiwa duniani kote?