6 Ombolezeni enyi wenyeji wa Foinike!Jaribuni kukimbilia Tarshishi.
7 Je, huu ndio mji wa furaha wa Tiro,mji ambao ulijengwa zamani za kale,ambao wakazi wake walikwenda kumiliki nchi za mbali?
8 Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro,mji uliowatawaza wafalme,wafanyabiashara wake walikuwa wakuu,wakaheshimiwa duniani kote?
9 Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi!Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote.Alifanya hivyo akiharibu kiburi chaona kuwaaibisha waheshimiwa wake.
10 Limeni sasa ardhi yenu enyi wakazi wa Tarshishi;maana hamna tena bandari kwa ajili ya meli kubwa.
11 Mwenyezi-Mungu ameunyosha mkono wake juu ya bahari,amezitetemesha falme;ametoa amri kuziharibu ngome za Kanaani.
12 Alisema: “Ewe binti Sidonihutaweza kufanya sherehe tena;hata ukikimbilia Kupro,huko nako hutapata pumziko!”