1 Sasa Mwenyezi-Mungu anaiharibu duniana kuifanya tupu.Atausokota uso wa duniana kuwatawanya wakazi wake.
2 Kila mtu atapatwa na mambo yaleyale:Mtu wa kawaida na kuhani;mtumwa na bwana wake;mjakazi na bibi yake;mnunuzi na mwuzaji;mkopeshaji na mkopaji;mdai na mdaiwa.
3 Dunia itaharibiwa kabisa na kuangamizwa;Mwenyezi-Mungu ametamka hayo.
4 Dunia inakauka na kunyauka;ulimwengu unafadhaika na kunyauka;mbingu zinafadhaika pamoja na dunia.