4 Dunia inakauka na kunyauka;ulimwengu unafadhaika na kunyauka;mbingu zinafadhaika pamoja na dunia.
5 Watu wameitia najisi duniamaana wamezivunja sheria za Mungu,wamezikiuka kanuni zake,wamelivunja agano lake la milele.
6 Kwa sababu hiyo laana inaitokomeza dunia,wakazi wake wanateseka kwa makosa yao.Wakazi wa dunia wamepungua,ni watu wachache tu waliosalia.
7 Mizabibu inanyauka,divai inakosekana.Wote waliokuwa wenye furahasasa wanasononeka kwa huzuni.
8 Mdundo wa vigoma umekoma,nderemo na vifijo vimetoweka;midundo ya vinubi imekomeshwa.
9 Hakuna tena kunywa divai na kuimba;mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji.
10 Mji uliohamwa umejaa uharibifu;kila nyumba imefungwa asiingie mtu.