26 “Je, hujasikia ewe Senakeribu kwambanilipanga jambo hili tangu zamani?Ninachotekeleza sasa nilikipanga zamani.Nilikuweka uifanye miji yenye ngomekuwa rundo la magofu.
27 Wakazi wake wakiwa wameishiwa nguvu,wametishika na kufadhaika.Wamekuwa kama mimea shambani,kama nyasi changa shambani,kama majani yaotayo juu ya paaau kama ngano kabla hazijakomaaambazo hunyauka upepo mkavu uvumapo.
28 Lakini, nakujua wewe Senakeribu;najua kila unachofanya na kuacha kufanya;najua mipango yako dhidi yangu.
29 Kwa vile umefanya mipango dhidi yanguna nimeusikia ufidhuli wako,nitatia ndoana yangu puani mwako,na lijamu yangu kinywani mwako.Nitakurudisha njia ileile uliyojia.”
30 “Na hii ndiyo itakuwa ishara kwako Hezekia: Mwaka huu na mwaka ujao mtakula kinachomea chenyewe bila kupandwa. Lakini katika mwaka wa tatu mtapanda na kuvuna mavuno; mtapanda mizabibu na kula matunda yake.
31 Wale watakaobaki katika ukoo wa Yuda wataongezeka na kuwa wengi kama vile mti unavyotoa mizizi yake udongoni na kuzaa matunda juu.
32 Maana kutakuwa na watu watakaosalia huko Yerusalemu; naam, huko mlimani Siyoni kutakuwako watu wachache watakaosalimika.” Mwenyezi-Mungu wa majeshi amedhamiria kukamilisha hayo.