1 Mungu wenu asema:“Wafarijini watu wangu,nendeni mkawafariji.
2 Semeni na wenyeji wa Yerusalemu kwa upole,waambieni kwamba utumwa wao umekwisha,wamesamehewa uovu wao.Mwenyezi-Mungu amewaadhibu maradufukwa sababu ya dhambi zao zote.”
3 Sauti ya mtu anaita jangwani:“Mtayarishieni Mwenyezi-Mungu njia,nyosheni barabara kuu kwa ajili ya Mungu wetu.
4 Kila bonde litasawazishwa,kila mlima na kilima vitashushwa;ardhi isiyo sawa itafanywa sawa,mahali pa kuparuza patalainishwa.