1 “Haya! Kila mwenye kiu na aje kwenye maji!Njoni, nyote hata msio na fedha;nunueni ngano mkale,nunueni divai na maziwa.Bila fedha, bila gharama!
2 Mbona mnatumia fedha yenukwa ajili ya kitu kisicho chakula?Ya nini kutoa jasho lenu kwa kitu kisichoshibisha?Nisikilizeni mimi kwa makini,nanyi mtakula vilivyo bora,na kufurahia vinono.
3 “Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu;nisikilizeni, ili mpate kuishi.Nami nitafanya nanyi agano la milele;nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi.
4 Mimi nilimfanya kiongozi na kamanda wa mataifaili yeye anishuhudie kwa watu wa mataifa.
5 Sasa utayaita mataifa usiyoyajua,watu wa mataifa yasiyokutambua watakujia mbio,kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeliniliyekufanya wewe utukuke.”