3 “Tegeni sikio enyi watu wangu, mje kwangu;nisikilizeni, ili mpate kuishi.Nami nitafanya nanyi agano la milele;nitawapeni fadhili nilizomwahidi Daudi.
4 Mimi nilimfanya kiongozi na kamanda wa mataifaili yeye anishuhudie kwa watu wa mataifa.
5 Sasa utayaita mataifa usiyoyajua,watu wa mataifa yasiyokutambua watakujia mbio,kwa sababu yangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;kwa sababu yangu mimi Mtakatifu wa Israeliniliyekufanya wewe utukuke.”
6 Mtafuteni Mwenyezi-Mungu wakati bado anapatikana,mwombeni msaada wakati yupo bado karibu.
7 Waovu na waache njia zao mbaya,watu wabaya waachane na mawazo yao mabaya;wamrudie Mwenyezi-Mungu apate kuwahurumia,wamwendee Mungu wetu maana atawasamehe.
8 Maana, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mawazo yangu si kama mawazo yenu,wala njia zangu si kama njia zenu.
9 Kama vile mbingu zilivyo mbali na dunia,ndivyo njia zangu zilivyo mbali na zenu,na mawazo yangu mbali na mawazo yenu.