1 Inuka ee Siyoni uangaze;maana mwanga unachomoza kwa ajili yako,utukufu wa Mwenyezi-Mungu unakuangaza.
2 Tazama, giza litaifunika dunia,giza nene litayafunika mataifa;lakini wewe, Mwenyezi-Mungu atakuangazia,utukufu wake utaonekana kwako.
3 Mataifa yataujia mwanga wako,wafalme waujia mwanga wa pambazuko lako.
4 Inua macho utazame pande zote;wote wanakusanyika waje kwako.Wanao wa kiume watafika toka mbali,wanao wa kike watabebwa mikononi.
5 Utaona na uso wako utangara,moyo wako utasisimka na kushangilia.Maana utajiri wa bahari utakutiririkia,mali za mataifa zitaletwa kwako.
6 Makundi ya ngamia yataifunika nchi yako,naam, ndama wa ngamia kutoka Midiani na Efa;wote kutoka Sheba watakuja.Watakuletea dhahabu na ubani,wakitangaza sifa za Mwenyezi-Mungu.