1 Mwenyezi-Mungu asema;“Nilikuwa tayari kujioneshakwao wasiouliza habari zangu.Nilikuwa tayari kuwapokeawale wasionitafuta.Nililiambia taifa ambalo halikuomba kwa jina langu:‘Nipo hapa! Nipo hapa!’
2 Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu waasi,watu ambao hufuata njia zisizo sawa,watu ambao hufuata fikira zao wenyewe.
3 Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi;hutambikia miungu yao katika bustani,na kuifukizia ubani juu ya matofali.
4 Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku.Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu.
5 Huwaambia wale wanaokutana nao:‘Kaeni mbali nami;msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’Watu hao wananikasirisha mno,hasira yangu ni kama moto usiozimika.
6 “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni,sitanyamaza bali nitawafanya walipe;nitawafanya walipe kwa wingi.
7 Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yaowayalipie na maovu ya wazee wao.Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani,wakanitukana mimi huko vilimani.Nitawafanya walipe kwa wingi,watayalipia matendo yao ya awali.”