20 Lakini mkikaidi na kuniasi,mtaangamizwa kwa upanga.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”
21 Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.
22 Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.
23 Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.
24 Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
25 Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.
26 Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanzana washauri wenu kama pale awali.Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”