21 Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.
22 Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.
23 Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.
24 Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
25 Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.
26 Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanzana washauri wenu kama pale awali.Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”
27 Mji Siyoni utakombolewa kwa haki,uadilifu utawaokoa watakaotubu humo.