18 Mishale yao itawaua vijana,hawatakuwa na huruma kwa watoto,wala kuwahurumia watoto wachanga.
19 Babuloni johari ya falme zotena umaarufu wa kiburi cha Wakaldayoutakuwa kama Sodoma na Gomora,wakati Mungu alipoiangamiza.
20 Kamwe hautakaliwa tena na watu,watu hawataishi humo katika vizazi vyote.Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo,wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
21 Badala yake watakuwamo wanyama wakali wa porini,bundi watajaa katika nyumba zake.Mbuni wataishi humo,na majini yatachezea humo.
22 Mbwamwitu watalia ndani ya ngome zake,mbweha wataonekana ndani ya nyumba zao za anasa.Wakati wa Babuloni umekaribia,wala siku zake hazitaongezwa.”