3 watu wengi wataujia na kusema,“Njoni tupande mlima wa Mwenyezi-Mungu,twende nyumbani kwa Mungu wa Yakobo,apate kutufundisha njia zake,nasi tuishi kadiri ya mwongozo wake.Maana sheria itakuja kutoka Siyoni;neno la Mwenyezi-Mungu kutoka Yerusalemu.”
4 Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifaatakata mashauri ya watu wengi.Watu watafua panga za vita kuwa majembena mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea.Taifa halitapigana na taifa linginewala hayatafanya tena mazoezi ya vita.
5 Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni,tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu.
6 Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo.Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao,wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti.Wanashirikiana na watu wageni.
7 Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,hazina yao ni kubwa kupindukia.Nchi yao imejaa farasi,magari yao ya kukokotwa hayana idadi.
8 Nchi yao imejaa vinyago vya miungu,huabudu kazi ya mikono yao,vitu walivyotengeneza wao wenyewe.
9 Kwa hiyo, kila mtu ataaibishwa na kufedheheshwa.Usiwasamehe hata kidogo, ee Mungu!