10 Mji uliohamwa umejaa uharibifu;kila nyumba imefungwa asiingie mtu.
11 Kuna kilio barabarani kwa kukosa divai;shangwe yote imekoma,furaha imetoweka duniani.
12 Mji ni magofu matupu;malango yake yamevunjwavunjwa.
13 Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituniau tini chache tu juu ya mtinibaada ya kumaliza mavuno,ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote:Watu wachache watabakia hai.
14 Watakaosalia watapaza sauti,wataimba kwa shangwe.Kutoka magharibi watatangaza ukuu wa Mwenyezi-Mungu,
15 nao wakazi wa mashariki watamsifu.Watu wa mbali watalisifujina la Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.
16 Tunasikia nyimbo za sifa kutoka miisho ya dunia,nyimbo za kumsifu Mungu aliye mwadilifu.Lakini mimi ninanyongonyea,naam, ninanyongonyea.Ole wangu mimi!Wasaliti wanaendelea kuwa wasaliti,usaliti wao unazidi kuwa mbaya zaidi.