18 Atakayeikimbia hofu atatumbukia shimoni;atakayetoka shimoni atanaswa mtegoni.Madirisha ya mbinguni yamefunguliwa,misingi ya dunia inatikisika.
19 Dunia inavunjikavunjika,inapasuka na kutikiswatikiswa.
20 Inapepesuka kama mlevi,inayumbayumba kama kibanda.Imelemewa na mzigo wa dhambi zakenayo itaanguka wala haitainuka tena.
21 Siku ile Mwenyezi-Mungu ataliadhibu jeshi la anganikadhalika na wafalme wa duniani.
22 Wote watakusanywa kama wafungwa shimoni;watafungwa gerezani pamoja kwa miaka mingi,na baada ya muda huo atawaadhibu.
23 Kisha mwezi utaaibishwa,nalo jua litaona aibu kuangaza,kwa kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshiatatawala huko Yerusalemu katika mlima Siyoni;ataonesha wazee wa watu wake utukufu wake.