7 Mizabibu inanyauka,divai inakosekana.Wote waliokuwa wenye furahasasa wanasononeka kwa huzuni.
8 Mdundo wa vigoma umekoma,nderemo na vifijo vimetoweka;midundo ya vinubi imekomeshwa.
9 Hakuna tena kunywa divai na kuimba;mvinyo umekuwa mchungu kwa wanywaji.
10 Mji uliohamwa umejaa uharibifu;kila nyumba imefungwa asiingie mtu.
11 Kuna kilio barabarani kwa kukosa divai;shangwe yote imekoma,furaha imetoweka duniani.
12 Mji ni magofu matupu;malango yake yamevunjwavunjwa.
13 Kama vile zeituni chache tu juu ya mzeituniau tini chache tu juu ya mtinibaada ya kumaliza mavuno,ndivyo itakavyokuwa katika nchi zote:Watu wachache watabakia hai.